Mina Man of the Match kwa Upande wa Colombia World Cup 2018

UTANGULIZI

Hakika kamwe huwezi kuzungumzia mechi ya jana baina ya Colombia na England bila kumtaja Yerry Fernando Mina mchuezaji wa kulipwa toka timu ya taifa ya Colombia.Waweza jiuliza kafanya nini??.Yeye ni nani???.Fuatana nami uelimike hapa hapa soma kidigitali...

KIINI

Yerry Fernando Mina ni nani??.Wow! jibu lake ni rahisi sana ni mchezaji wa timu ya taifa ya Colombia.Je, alizaliwa wapi na ni mwaka gani? Mina amezaliwa Guachene ,Colombia tarehe 23,Septemba 1994 na sasa ana miaka 23.Mmmh! sasa anachezea klabu gani??.Mina anachezea klabu ya Barcelona kama beki au mlinzi wa kati.Ana urefu wa 1.95 m pia uzito wake ni 94 kg.

Ahhaaa! kumbe! sasa alifanya nini katika mechi ya jana??.Mina aliweza kuifungia timu yake ya Colombia goli 1 la kusawazisha katika  dakika 5' za nyongeza baada ya dakika 90 kuisha na hivyo kuifanya Colombia kufikia hatua ya kupiga penait.Je,ana magoli mangapi katika kombe la dunia 2018??.Mina amefunga magoli 3 katika michuano hii ya kombe la dunia Russia 2018.

HITIMISHO

Huyo ndiye Mina mchezaj wa Colombia mwenye  jezi namba 13 mgongoni. Je,una maoni gani kwake?? toa maoni.Endelea kutembelea soma kidigitali blog huelimike kuhusu michezo,masomo ya sekondari kwa njia ya video,past papers,ratiba za form 4,form 2 za mitihani ya taifa 2018 n.k.Karibu

Maoni