UTANGULIZI
Waooh! France kwa ushindi mliojiandikia jana kwa kufunga magoli 4 dhidi ya Argentina waliofunga magoli 3 katika kuwania kombe la dunia 2018 Russia.Katika ushindi wa France umeletwa na uhodari wa kikosi cha Ufaransa lakini huwezi puuzia kuelezea uwezo wa Kylian Mbappe .Je, wa mfahamu Kylian Mbappe??.Fuatana nami ili umfahamu mchezaji huyu....
KIINI
Kylian Mbappe ni mchezaji wa kulipwa mwenye ujuzi na weledi katika ulingo wa mpira duniani.Alizaliwa mnamo mwaka 1998, Desemba 20 huko katika jiji la Parisi Ufaransa kwa sasa ana miaka 19.Ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa.Waweza jiuliza je,anacheza timu klabu gani??.Kylian Mbappe anachezea klabu ya Paris Saint Germain(PSG) akitokea klabu ya Monaco kwa mkopo.
Swali jingine waweza jiuliza anacheza namba ngapi?.Jibu ni kuwa Kylian Mbappe anacheza mbele namba 10.Je,ana urefu kiasi gani na anauzito kiasi gani???.Mbappe amebarikiwa kuwa na urefu wa futi 5'10 sawa na (1.78 m) na uzito wake ni 73 kg.
Ehee! amefunga magoli mangapi katika mechi ya Ufaransa na Argentina???.Mbappe amefunga magoli mawili(2) katika mechi hii na kuifanya Ufaransa ifuzu katika kuingia hatua inayofuatia katika kombe la dunia.
HITIMISHO
Huyo ndiyo Kylian Mbappe mchezaji mwenye umri mdogo ambaye ni mchezaji mwenye ujuzi mkubwa katika ulimwengu wa soka .Endelea kufuatilia habari za michezo za kombe la dunia 2018 hapa hapa somakidigitali jisali sasa.
Maoni
Chapisha Maoni