FAHAMU MFUMO WA ELIMU TANZANIA


UTANGULIZI

Je, wewe wafahamu mfumo wa elimu Tanzania?.Mathalani elimu ni nini?.Mimi najua kwanza wapaswa fahamu kuwa elimu ni usambasaji au usafirishaji wa maarifa na ujuzi kutoka kwa mtu mwenye maarifa au ujuzi fulani kwenda kwa mtu mwingine.Maarifa hayo hupatikana kwa kufundishwa,kuiga na kadhalika.Mfumo wa elimu ni namna ambavyo elimu imepangiliwa na uko tofauti baina ya nchi moja na nyingine.

KIINI

Kwa Tanzania tuna mfumo wa elimu ambao umegawanyika katika muundo huu:-

Elimu ya msingi ;muundo huu umegemezwa katika sehemu kuu mbili yaani  kwanza elimu ya awali ambayo huusisha wanafunzi mwenye umri kuanzia miaka 5 na husoma kwa miaka miwili.Pili ni elimu ya shule ya msingi ambapo mwanafunzi huanza na miaka saba(7) na husoma kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba.Kwa takwimu za 2017 idadi ya wanafunzi wa shule za msingi  ni 9,317,410 kati ya hao wavulana ni 4,629,027 sawa na 49.7% ,4,688,383 sawa na 50.3% ni wasichana.Shule hizi humilikiwa na serikali na watu binafsi.Ikumbukwe kuwa idadi ya wanafunzi hukuwa kila mwaka.




 Elimu ya sekondari;Baada ya mwanafunzi kumaliza elimu ya msingi huweza kujiunga na elimu ya sekondari kwa miaka minne(4) yaani kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.Idadi ya wanafunzi  ni 1,909,017 kwa takwimu za 2016-17 kati yao 947,486 sawa na 49.6% ni wavulana na 961,531 sawa na 50.4% ni wasichana. Idadi hii hubadilika kila mwaka  na umiliki wa shule ni kuwa zipo zinazomilikiwa na serikali na za watu binafsi .





Elimu ya vyuo;Wanafunzi huweza jiunga na vyuo mbali mbali yaani vya ufundi, afya na kadhalika.Vyuo huweza kumilikiwa na serikali na watu binafsi.Wanafunzi huweza kusomea cheti na hata diploma katika fani tofauti tofauti.



Elimu ya Chuo;Ni maarufu kama chuo kikuu ambapo kuna vyuo vingi tu ambavyo humilkiwa na serikali na watu binafsi.Wanazuoni huweza kusoma kuanzia miaka mitatu(3) na kuendelea kutegemeana na fani husika.Elimu hii hutolewa kwa ngazi tofauti tofauti ya degree ya kwanza, ya pili,doctorate na PHD.



HITIMISHO 
Elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa.Serkali na taasisi binafsi ichunguze kwa kina changamoto mbali mbali katika elimu na itafutie suluhisho chanya ili kujenga Tanzania mpya ya Viwanda yenye wasomi wenye weledi katika sekta tofauti tofauti kwa maendeleo ya Taifa .
 Chanzo.: Tamisemi

Maoni