ZUIA UCHAFUZI MAZINGIRA SASA





UTANGULIZI
Dear umeshawahi kujiuliza mazingira nini maana yake? eeeh! yanafaida gani kwa mwanadamu na ni namna gani uyatunze?, Je, siku ya mazingira duniani ni nini?.Teeh! tehee!! nacheka kwa furaha.Mmmh! majawabu yake ni rahisi mazingira ni kila kitu kinachotuzunguka wanadamu yaani miti,wanyama na kadhalika,mazingira ukiyatunza yaana faida tele kama vile uwepo wa maji safi,hewa safi, upatikanaji wa nishati kwa urahisi kama vile nishati ya jua,upatikanaji wa chakula cha kutosha mwaka mzima na uzuri wa dunia huonekana kama tukitunza mazingira.
 Siku ya mazingira duniani je?, ni  siku maalumu ambayo dunia nzima huadhimisha kwa kutunza mazingira kila mwaka huazimishwa tarehe 5,June mwaka huu tuna adhimisha katika nchi ya india.
KIINI
Ahaa!kwa mwaka huu dunia nzima imewekeza katika kampeni hizi za kimazingira ambazo ningependa nikushirikishe mwanadamu mwenzangu ambazo ni:-
  1. Zuia matumizi ya plastic- ili kuifanya dunia kuwa ni sehemu ya kutamani kuishi muda wote zuia matumizi ya plastic shuleni,vyuoni,majumbani,sokoni na kadhalika.
 2.Zuia uchafuzi  wa mazingira - mara nyingi huua watu wengi zaidi duniani kwa magonjwa mbalimbali .
3.Safisha bahari- bahari tukisafisha tunagengeneza mazingira rafiki ya kupata samaki,kutunza ndege wa baharini ambao wanakufa kwa kasi zaidi ifikapo 2050 kama hatuta safisha bahari zetu.


4.Wanyama kwa maisha- ni wajibu wa kila mwanadamu kutunza wanayama katika mapori yetu kwa kupiga vita dhidi ya ujangiri ili kulinda simba ,jaguar,kifaru,tembo na kadhali kwani wanyama ni fahari yetu tuwatunze.


5.Safisha anga- Piga vita shughuli zote zinazoharibu anga kwa kupunguza na hata kuondoa kabisa.Watoto wengi duniani hupoteza maisha kwa uchafuzi wa anga.
HITIMISHO
Chagua ni kampeni ipi uanayotaka kuifanya katika siku ya mazingira dunia comment au toa maoni.Tunza mazingira yakutunze
Chanzo; http://www.unevironmentday.global

Maoni