UBORA WA LIKIZO KWA WANAFUNZI



 UTANGULIZI
Maisha ya mwanafunzi au mwanazuoni siku zote yamezungukwa na harakati za masomo.Mimi nakumbuka maisha ya shule ya msingi ,sekondari na chuo yaliyoegemezwa katika kuamka asubuhi mapema alfajiri kuwahi shule au chuo,mijaribu(majaribio),mitihani ,course work  na mambo kede kede unachoka kabisa.Vipi wewe kwa upande wako niambie uzoefu wako?.Ila kinapofika kipindi cha likizo wow! nakipenda sana nafurahia sana je wewe?.

 KIINI
Ubora  wa likizo unategemea na mambo unayo yafanya wakati wa likizo yaani:-
  • Kutembelea ndugu na jamaa ; wengine tunakumbuka pale unapotoka chuo,shule kwenda nyumbani ukifika unatamani sana kutembelea kwa bibi ,babu, mjomba,shemeji,dada ,rafiki zako wa karibu majirani iwe ni mjini au vijijini ili kuwasabai.
  • Kufanya matembezi; hapa waweza toka nyumbani kwenda kutembelea sehemu mbalimbali kama vile mbuga za wanyama,vukweni(beach) na kadhalilka.
  • Kukaa karibu na familia;yaani kumalizia likizo nyumbani kukaa karibu na familia yako .Mimi napenda sana kukaa na familia yangu wakati wa likizo hasa christmass na kadha wa kadha.Mmmh! niambie wewe vipi kwa upande wako? niambie ..........
  • Kutoacha kabisa shughuli ulizozoea kufanya; tuliowengi kipindi cha likizo huwa tunasahau kabisaaa kama ni mwanafunzi husahau kabisa kusoma inashauriwa kuweza kusoma soma ili kuzuia hali ya ugumu wa kuanza  kuzoea kusoma upya pindi likizo inapoisha.Wakati huu wengine hutumia kwa masoma ya ziada ya sayansi na sanaa.
HITIMISHO
Likizo time ina faida nyingi sana kama vile huleta furaha,faraja kutoka katika heka heka za masomo,mapumziko,kupata nguvu mpya ili  kuanza muda mpya wa masomo au kazi.Toa maoni yako paza sauti.
 Chanzo;https;//www.indiancelebrating.com
 

Maoni