Itambue Njia Rahisi Ya Kupata Simu Yako Ya Android iliyopotea

UTANGULIZI

Inauma sana kuibiwa au kupoteza simu yenye nyaraka au taarifa  zako za muhimu za kikazi ,binafsi,kibiashara n.k.Mara kwa mara vibaka wanatuibia simu madirishani lakini hatujui tufanye nini ili tuweze kupata simu zetu .Je,ulishawahi ibiwa au poteza simu na haujaipata mpaka sasa na haujui utumie njia gani kuipata?.Usihofu ambatana nami ili uweze jua njia rahisi ya kupata simu yako ya android iliyopotea

KIINI

Kuna hatua 3 kuu za kufuata ili upate simu yako iliyoibiwa au potea kwa urahisi ambazo ni:
  1. Tafuta / Chapa android.com/find katika google au search engine nyingineyo
  2. Kisha andika email na password ambayo ulikuwa unaitumia katika simu iliyopotea au kuibiwa
  3. Tazama mahali ilipo ni uchaguzi wako kuipigia ,kuizima au kwenda kutoa taarifa polisi kwa ajili ya kumkamata mwizi.
Kwa msaada zaidi tazama video hii itakayokusaidia kutambua namna ya kupata simu yako ya android iliyopotea bofya katikati ya kitufe chekundu karibu tazama











HITIMISHO

Naam,umetazama rafiki na umejua njia raisi ya kupata simu yako ya android iliyopotea?.Endelea kutazama soma kidigitali blog na somakidigitali You tube channel tukuelimishe kuhusu masomo ya darasani sekondari kwa njia ya video,michezo,teknolojia n.k dont miss it.

Maoni

Chapisha Maoni