FAHAMU MAMBO 6 YA MSINGI YA KUZINGATIA KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA JKT 2018

  UTANGULIZI
Mimi ninatoa pongezi zangu za dhati toka kwenye uvungu wangu wa moyo kwa wale  wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita 2018 kwa kupata bahati hadimu ya kuchaguliwa  na JKT kwa mujibu wa sheria.Pia shukurani zangu za dhati  saana ni kwa jeshi letu la JKT kwa kazi kubwa  nzuri  wanazofanya kwa mustakabali wa taifa letu la Tanzania.Mola awabariki saana .
KIINI
Kuna mambo sita ya msingi ambayo kila wanafunzi aliyechakuliwa 2018 anapaswa kuyatilia maanani na kuyatekeleza kwa weredi ambayo ni kama yafuatayo:-

  1.   Kwa aliyechaguliwa anapaswa kujigharamia nauli ya kumfikisha katika kambi husika aliyochaguliwa.
  2. Anapaswa awe na bukta ya rangi ya dark blue yenye mpira kiunoni ,iliyo na mfuko mmoja nyuma,urefu inayoishia magotini isiyo na zipu kwa upande wasichana iwe na lastic magotini.
  3. Raba za michezo rangi ya blue bahari.  
  4. Soksi ndefu nyeusi.
  5. Tracki suti ya rangi ya kijani au bluu.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa wale waliochaguliwa kwenye kambi zenye mikoa ya baridi.

  HITIMISHO
Napenda kukutakia maandalizi mema katika kuhudhuria mafunzo haya yenye lengo la dhati la kuandaa taifa la vijana wazalendo wenye nia chanya ya kujenga taifa letu lisonge mbele katika nyanja zote  za maisha kiuchumi,kijamii na hata kisiasa. Asantee sana kwa kusoma makala hii fupi.
 NB: Picha hizo ni za mfano tu  na si halisi.
 Chanzo: JKT. https://www.jkt.go.tz

Maoni